LIPUMBA AWASIHI JUVICUF WASIANDAMANE, WAKUBALIANA NAYE


maandamano ya vijana cuf, lipumbamaandamano cuf, maandamano lipumba, maandamano juvicufjuvicuf, maandamano

Polisi wakiwa wamejiimarisha kuzuia maandamano ya Vijana wa CUF eneo la Buguruni.

maandamano juvicuf, lipumba

Wananchi wakijadiliana kuhusu tukio hilo.

MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF)  Profesa Ibrahim Lipumba leo amewasihi Jumuiya ya Vijana wa CUF(JUVICUF) kusitisha maandamano kama jeshi la polisi lilivyoagiza .
Akizungumza leo katika ofisi za chama hicho zilizopo Buguruni, jijini Dar e s Salaam,  amesema kuwa vijana hao waache kuandamana kwa sababu kunaweza kutokea madhara makubwa ikiwa ni pamoja na  kupigwa risasi, vifo na kadhalika.
Alisisitiza waache kuandamana ingawa dhamira yao  ya kuitaka  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iongeze siku za uandikishwaji wa upigaji kura  kutoka siku saba hadi 14 ina mantiki kwa Watanzania wote.
JIVICUF walikuwa waandamane kusisitiza, miongoni mwa mambo mengine, kuhusu uvunjwaji  wa haki za binadamu nchini na dosari za uandikishaji wapiga kura.
(Habari/Picha: kwa hisani ya GPL)


No comments:

Post a Comment

Peruzi Kurasa.

Designed By Seo Blogger Templates Published.. Blogger Templates