NDOA YA TEMBA YAPUMULIA MASHINE



NDOA ya msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Amani James 'Temba' inadaiwa kupumulia mashine kutokana na madai ya kuwepo kwa usaliti baina yao.
Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Amani James 'Temba' akiwa na mke wake siku ya ndoa yao.
Habari kutoka kwa chanzo kilicho karibu na wanandoa hao wanaoishi wilayani Temeke, kinasema kumekuwa na mgogoro wa muda mrefu baina ya watu hao, kila mmoja akimtuhumu mwenzake kusaliti, jambo linaloonyesha wakati wowote ndoa yao inaweza kusambaratika.
"Jamaa hayuko 'peace' kabisa na ndoa yake, yaani kila siku ni mgogoro, wife wake anamshutumu mshkaji kuwa msaliti kwa wanawake wengine na mke naye anatuhumiwa hivyohivyo ili mradi hakuna amani kabisa.
Inaonekana kuna tatizo kubwa," kilisema chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.
Gazeti hili halikuweza kuwapata wanandoa hao kutokana na simu zao kutopatikana, lakini wakati linakwenda mitamboni, lilipata taarifa za kufikishwa mahakamani kwa Mheshimiwa Temba, ambaye anashtakiwa kwa kosa la kutishia kuua, kitendo alichokifanya kwa Godfrey Deogratius anayemtuhumu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe.
Soma zaidi...

Diamond Platnumz na Ambwene Yessayah 'AY' Watesa Chati za muziki Majuu


Muziki wa Tanzania upo mahali pazuri kwa sasa. AY, Diamond Platnumz na wasanii wengine wanaiwakilisha vyema nchi yetu kimataifa.

Wasanii hao wamekamata nafasi za kwanza wiki hii kwenye top ten za chart za muziki wa Afrika katika vituo vikubwa viwili vya runinga.

Diamond Platnumz amekamata nafasi ya kwanza kwenye African Top 10 ya Trace International na wimbo wake Ntampata Wapi.

Naye AY amekamata nafasi ya kwanza kwenye chart ya Africa Rox Countdown ya Soundcity kwa wimbo wa 'Touch Me' aliowashirikisha Sean Kingston na Ms Triniti
Soma zaidi...

Shilole Awafungukia Marafiki Wanaotaka Kumgombanisha Na Nuh Mziwanda!





MSANII wa muziki na mwigizaji wa filamu za Bongo, Zuwena Mohamed 'Shilole', ameamua kuweka wazi chanzo cha migogoro yake na mumewe mtarajiwa, Nuh Mziwanda kuwa ni marafiki.

Shilole alidai kuwa mara nyingi wamekuwa wakigombana, lakini chanzo kikiwa ni maneno ya uchonganishi kutoka kwa marafiki zao wa karibu ambao wana lengo la kuwatenganisha. Mwanadada huyo alidai kutokana na hali hiyo, hivi sasa ameamua kutowahusisha suala lolote linalohusu maisha yake ili kupunguza migogoro ya mara kwa mara baina yao.
Alisema wale walio karibu yao ndio wanaochangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa migogoro kwenye mahusiano yao, ukizingatia hivi sasa wapo kwenye harakati za kufunga ndoa baada ya wazazi wa pande zote kukubali uhusiano wao.

"Tumegundua kuwa mashoga ndio wanaotugombanisha, kwani kila mara mchumba wangu anapewa taarifa zinazonihusu mimi huku hao hao wakiniletea habari zake, jambo hili limesabababisha nisihitaji tena marafiki wengi wao ni wanafiki,"alisema.
Soma zaidi...

TIKO: NATAKA MTOTO WA PILI, WA KUNIPA MIMBA SINA




Na Hamida Hassan/Ijumaa
Staa wa filamu za Kibongo, Tiko Hassan amesema kuwa anatamani kupata mtoto wa pili kwa sababu mtoto wake wa kwanza amefikisha miaka 10, tatizo hana wa kuzaa naye.

Staa wa filamu za Kibongo, Tiko Hassan.

Akipiga stori na Ijumaa Tiko alisema yeye ni 'mgonjwa' wa watoto wachanga na anahisi sasa ni muda muafaka ila tatizo mwanaume aliyenaye hana mpango wa kupata mtoto.
"Yaani acha tu, mpenzi niliyenaye naona kama hajajiandaa maana hata nikiongelea ishu ya kubeba mimba, naona ananipotezea lakini kiukweli nahitaji mtoto wa pili," alisema Tiko.
Soma zaidi...

LULU, WOLPER WAONESHANA JEURI YA PESA



Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Elizabeth Michael 'Lulu'. 


TAMBO ZA NANI ZAIDI?

Sakata la kupangishiwa nyumba za kifahari na wanaume linazidi kuchukua sura mpya kwa mastaa wa kike ndani ya tasnia ya sinema za Kibongo ambapo safari hii mastaa wawili, Elizabeth Michael 'Lulu' na Jacqueline Walper ' Wolper' Massawe wanadaiwa kuoneshana jeuri ya mabwana wakipima ni yupi mwenye mshiko zaidi huku akina Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja ambao awali walikuwa juu wakipotezwa. 
Uchunguzi wa Ijumaa umebaini kwamba, kumekuwa na kasumba ya baadhi ya mastaa hao kutambiana kuwa ni nani zaidi anayemiliki bwana mwenye mawe au mshiko kuliko wengine. 
Ilidaiwa kwamba, baada ya Lulu kuripotiwa kupangishiwa bonge la jumba la kifahari na milionea maarufu wa jijini Arusha lililopo maeneo ya Mbezi-Beach jijini Dar, Wolper naye anadaiwa kujibu mapigo kwa kupangishiwa mjengo wa maana na bwana'ke uliopo maeneo hayohayo.


Kwa mujibu wa vyanzo vyetu ambavyo ni watu wa karibu wa mastaa hao, kwa sasa wawili hao ni moto wa kuotea mbali kwani kila mmoja amepata bwana mwenye 'mpunga' mrefu. 

WOTE WANALIPA SH. MIL. 30 
Ilidaiwa kwamba, kama ilivyokuwa kwa Lulu, Wolper naye analipiwa nyumba hiyo kiasi cha dola za Kimarekani 1,500 kwa mwezi (zaidi ya Sh. milioni 2.4) karibia Sh. milioni 30 kwa mwaka.

Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Jacqueline Walper.

 CHUMBA KAMA BOUTIQUE

Habari zilidai kwamba, kama ilivyo ya Lulu, nyumba hiyo aliyopangishiwa Wolper ina vyumba kibao vya kulala, ukumbi wa wageni, sehemu ya kulia chakula, mabafu, majiko n.k

Pia nje ya nyumba hiyo kuna eneo kubwa la bustani iliyopambwa kwa maua mazuri na eneo la kutosha la maegesho ya magari.
Pamoja na kupangishiwa mijengo hiyo ya kifahari ushuani, Lulu na Wolper wamekuwa wakioneshana jeuri ya magari waliyonunuliwa na mabilionea hao. 


MAGARI

Uchunguzi unaonesha kuwa Lulu ana mkoko aina ya Toyota Rav4 New Model wenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 30.Kwa upande wake Wolper anasukuma ndinga aina ya Toyota Prado, nalo lina thamani ya zaidi ya Sh. milioni 30.

Jumba la kifahari alilopangishiwa Elizabeth Michael 'Lulu'.


 WATOFAUTIANA VITU VICHACHE

Habari za 'kiubuyu' zinadai kwamba wawili hao wanapishana vitu vichache mno kama vile aina ya mawigi na aina ya maisha (life style) ambapo bwana wa Wolper amempiga 'stop' kuigiza lakini bado Lulu anapiga mzigo. 

"Lulu na Wolper wamelamba bingo za nguvu na bahati nzuri wanaonekana wote kupata mabwana wasiokuwa na sifa."Kwa mfano, Lulu pamoja na kuishi katika maisha mazuri bado anasomeshwa na tayari ameshakamilishiwa ujenzi wa nyumba yake ambayo juzikati alimkabidhi mama yake kama zawadi. 

Jumba la kifahari alilopangishiwa Jacqueline Walper.

 WOLPER AKOSWA, MAJIRANI WAFUNGUKA

Ijumaa lilimtafuta Wolper kupitia simu yake ya mkononi lakini iliita bila kupokelewa. Mwandishi wetu alifika mtaa anaoishi Wolper, akagonga sana geti lakini halikufunguliwa.Hata hivyo, majirani wa staa huyo wamedai kuwa amekuwa akionekana akiingia na kutoka akiwa ndani ya gari hilo aina ya Toyota Prado. Jitihada za kumtafuta zinaendele
Soma zaidi...

Lulu Ayashukia Magazeti ya Udaku, VISA na LETE MAMBO


Mrembo na mwigizaji wa filamu, Elizabeth Michael 'Lulu' leo ameamua kuwapa makavu laivu magazeti hayo kwa kile ambacho Lulu anadai wamekuwa wakimbandika kwenye kurasa zao ya mbele kila leo kwa stori za kuungaunga.

"Okay...Acha nitoe PROMO bila Malipo tu maana inawezekana watu wana uhitaji...
Kwahyo kuna Magazeti yanaitwa VISA Na LETE MAMBO (tutambue uwepo wao kwanza) Sasa Sina uhakika kama ni masharti ya Boss zao Au ni sheria yao kutopitisha muda bila sura yangu kwenye magazeti yao tena Kwa story za kujitungia tu...Sitaki mnidhihirishie Kwamba bila SURA YANGU kwenye makaratasi yenu biashara haifanyiki....mtajiuliza Kwann nimekuja kuwaweka insta,mnajua sababu....mnajifanya ni ma bingwa wa kuchukua Habari kwenye mitandao Ya kijamii Na kuziboresha kwa uongo...Ichukueni na HII basi....!!

Kama kweli mna uhakika hata bila sura yangu kwenye makaratasi yenu kazi/biashara itakuwepo kama kawaida naomba mnidhihirishie hata ndani Ya miezi 3 tu....otherwise Basi niwe boss wenu mana bila mimi hamna mishahara...!

Endeleeni na madudu yenu...ila msije kukaa kwenye RIGHT ANGLE Mta Love show..!
NAJUA MTAPITA TU Cjui kama mna account humu ningewatag kbsa..!"-Lulu aliandika kwenye ukursa wake wa Instagram.

Bila shaka ujumbe umefika, ila nadhani hii pia kwao itakuwa stori pia.

Mzee wa Ubuyu
Soma zaidi...

Nuhu mziwanda aomba radhi kwa picha ya Ngono




Mwanamuziki Nuhu Mziwanda ambae ni mchumba wa mwanamuziki Shilole (Shishi baby) ameomba radhi jana kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kupost picha ambayo inaonyesha maungo ya ndani ya mpenzi wake huyo walipokuwa wakioga,picha hiyo ilimuonyesha Shilole akiwa kifua wazi.Kwa mujibu wa Nuhu Mziwanda amesema kuwa alipost picha hiyo ili apate Kiki kwa ajiri ya video yake mpya ya Zimataa ambayo bado haijatoka mpaka. 'Nuhu mziwanda aomba radhi kwa picha ya Ngono Mwanamuziki Nuhu Mziwanda ambae ni mchumba wa mwanamuziki Shilole (Shishi baby) ameomba radhi jana kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kupost picha ambayo inaonyesha maungo ya ndani ya mpenzi wake huyo walipokuwa wakioga,picha hiyo ilimuonyesha Shilole akiwa kifua wazi.Kwa mujibu wa Nuhu Mziwanda amesema kuwa alipost picha hiyo ili apate Kiki kwa ajiri ya video yake mpya ya Zimataa ambayo bado haijatoka mpaka.
Soma zaidi...

Peruzi Kurasa.

Designed By Seo Blogger Templates Published.. Blogger Templates