ALIYEVUNJWA TAYA AFANYIWA OPARESHENI, NDUGU WAOMBWA KUJITOKEZA



aliyevunjwa taya

Emmanuel Nelson Chitepete akiwa hospitalini.



Mwandishi wa Global TV Online & Mtandao, Gabriel Ng'osha, akikabidhi fedha kwa msimamizi wa wodi, Sista Masumbuko kutoka kwa Wasamaria wema waliochanga ili kumtibu mgonjwa huyo.
KIJANA Emmanuel Nelson, mkazi wa Tabata-Relini, jijini Dar es Salaam, ambaye aliokotwa na polisi wa kituo cha Pangani, Ilala, wiki kadhaa zilizopita  akiwa amevunjwa taya na watu wasiojulikana, wiki iliyopita alifanyiwa oparesheni na kufungwa waya taya lililovunjika.
Akizungumza na mtandao GPL, mmoja wa maofisa Ustawi wa Jamii jijini (hakutaka kutajwa jina lake) ambaye amekuwa akifuatilia kwa karibu matibabu ya kijana huyo alisema mgonjwa huyo anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa oparesheni.
Hata hivyo, aliongeza kwamba  bado hajatulia kiakili kwani kuna wakati anazungumza  vizuri na  wakati mwingine anakuwa kama anarukwa na akili.  Pamoja na hali hiyo, alisema, bado watoa huduma wanajitahidi kuendelea kumsaidia.
Ofisa huyo alisema Emmanuel  ameweza kumtaja baba yake mzazi  anayejulikana kwa jina la Nelson Andrew Chitepete, mkazi wa Chamwino, Area ''A'' Dodoma ambaye pia ni mfanyakazi mstaafu wa Tanzania Railway Company (TRC) Dodoma.
Alitoa wito kwa yoyote anayemfahamu Emmanuel, akiwemo mzee Chitepete wawasiliane na namba ya simu 0655207156 au kufika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Wodi ya Sewa Haji namba 23.
(Habari/Picha: Gabriel Ng'osha/GPL) 


No comments:

Post a Comment

Peruzi Kurasa.

Designed By Seo Blogger Templates Published.. Blogger Templates