ALIYEKUWA mchumba wa staa wa filamu za Kibongo, Rose Naduka, mwanamuziki Chiwa Malick Bandawe leo ametembelea ofisi za Global Publishers Ltd zilizopo Mwenge-Bamaga jijini Dar na kufanya mahojiano na Global TV Online.
Malick ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa Kundi la Bongo Fleva la TNG amefunguka vitu kibao akianza na muziki, maisha yake, mahusiano na mipango yake ya baadaye.
Katika mahojiano hayo ambayo yataruka hivi karibuni kupitia Global TV Online, Malick amefunguka sababu ya kuachana na mchumba wake wa muda mrefu Rose Ndauka ambaye amezaa naye mtoto mmoja wa kiume.
Mwanamuziki huyo baada ya kuachana na mpenzi wake huyo, kwa sasa anaendelea na maisha yake kama kawaida.
(PICHA NA MUSA MATEJA / GPL)
No comments:
Post a Comment