WACHEZAJI SITA KATI YA WANAOFIKIRIWA KUIRITHI MIKOBA YA STEVEN GERRARD LIVERPOOL.



Tangu Steven gerrard athibitishe kuondoka Liverpool mwishoni mwa msimu huu wa majira ya joto ampbapo mkataba wake utakuwa unamalizika, kumekuwa na mawazo mengi na wasiwasi kuhusu Liverpool baada ya Gerrard.
 Wengi wametoa maoni yao kuwa Liverpool itakuwa inaikosa 'hirizi' yake kubwa kutokana na uongozi wake mahiri bali pia itakuwa inampoteza mchezaji mkubwa ambaye aktika soko huria ana thamani kubwa ya pesa.

pamoja na machungu ya kumpoteza kiungo huyo mkongwe, uhalisia unabaki palepale, kwamba Liverpool inawabidi kutafuta mchezaji ambaye atafidia nafasi inayoachwa wazi na Gerrard-mwenyeuwezo wa kufunga na kutengeneza nafasi-mwezi julai.

Hawa ni wachezaji muhimu wanaoweza kuchukua nafasi ya Steven gerrard katika timu. Japokuwa hawawezi kuwa na uwezo sawa na gerrard lakini wanaweza kuwa na sifa alizokuwa nazo Gerrard kwa miakak mingi.

NDANI YA KLABU.

Pengine jibu bado ni siri ya brendan rodgers, lakini ukiachana na Gerrard na  Lucas Leiva, rogers hana kiungo mwingine aliyefikisha miaka 25.

Jordan Henderson

 Anaweza kuwa chaguo sahihi. Anatarajiwa kuchukua unahodha msimu ujao, akiwa na umri wa miaka 24 amechezea nafasi ya kiungo ndani ya Liverpool kwa miaka mitatu. ingawa alijituma kutwaa nafasi za juu msimu uliopita,pia amecheza kwa kujituma na ana pasi na nguvu ya kuwa suluhisho la muda mrefu.

Emre Can

Mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani. Emre (21) anatarajia kupata namba ya kudumu kikosi cha kwanza Anfield. Rodgers mwenyewe aliongelea uwezo wa Emre Can baada ya ushindi wake dhidi ya Burnley 'nafasi anayoipenda ni ya kujilinda zaidi, humiliki mchezo na huonekana kuwa na nguvu kwenye pambano.'

Jordan Rossiter.

Ni mmoja kati ya watarajiwa ndani ya Academy,kwa mara ya kwanza alionesha uwezo wake katika mechi ya kombe la Capital one dhidi ya Middlesbrough na alifunga ndani ya dakika 10. Ana uwezo mkubwa wa kulinda na kushambulia na pia anauwezo wa kuanzisha na kuzima mashambulizi kutokea nafasi yake ya kiungo wa kati.


KUSAJILI MAJINA MAKUBWA.

Kufuatia uamuzi wa Gerrard wa kuachana na klabu yake, kumekuwa na msisitizo wa wadau mbalimbali wa soka huko Uingereza kuitaka liverpool kununua 'jina kubwa' kiungo wa kiwango cha cha juu majira haya ya joto. Kwa kuwa Liverpool haitapata fungu la uhamisho kutoka kwa Gerrard inalifanya jambo hili kuwa na ugumu wake kidogo lakini kama wafarikiri kwa mapana, hii inaweza ikafaa. 

William Carvalho.

Kiungo wa Kireno anayedhaniwa kuwa nyota wa soka atakayefuatia nchini Ureno. Akiwa na miaka 22 tu, Carvaiho kiungo wa sporting Lisbon anahofia kudhoofukisoka ndani ya Lisbon, ukichanganya na mgogoro wa kifedha katika klabu yake inafikiriwa kuwa kuhamia kwenye ligi bora utakuwa ni uamuzi wa haraka kwake.

Sami Khedira.

Mshindi wa kombe la dunia tegemeo ndani ya Real Madrid. Amekuwa akihangaika na majeraha nyakati a hivi karibuni lakini ni tishio na moto wa kuotea mbali kwa wapinzani anapokuwa mzima. Ana pumzi kubwa na uwezo wa kupanda na kushuka.Mjerumani huyu anakuwa nafaida ya ziada kwa kuwa atakuwa huru msimu huu.

Paul Pogba.

nyota wa Juventus na mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa anayetawala Ligi ya Series A tangu ahamie Turin. Ana nguvu, pumzi na uwezo wa kumiliki mpira mguuni, Pogba anaweza kuwa chaguo linalotakiwa. Amehusishwa na kutaka kuhamia ligi kuu ya Uingereza kwa miezi kadhaa ya nyuma lakini anaweza kugharimu dau kubwa katika usajili.




No comments:

Post a Comment

Peruzi Kurasa.

Designed By Seo Blogger Templates Published.. Blogger Templates