Klabu ya Chelsea The Blues inaripotiwa kujiandaa kuushangaza ulimwengu wa soka kwa kutaka kumtwaa nyota wa Argentina na klabu ya Barcelona kwa kitita cha paundi milioni 200.
lionel Messi amekuwa akihusishwa na kutaka kuikacha kambi ya Nou Camp kwa siku za hivi karibuni na huenda akajikuta anaangukia katika dimba la Stamford Bridge.
Pia aliyemo katika mpango wa chelsea ni Paul pogba wa Juventus ambaye tayari Mashetani wekundu wamemtengea kiasi cha cha pauni milion 77 lakini Chelsea wapo tayari kupigania saini ya nyota huyo japokuwa Arsenal na Liverpool nao wanaonesha nyendo za kumnyatia.
Remirez anasepa na tayari juventus na Real Madrid wameonesha nia ya kumyakua Mbrazil huyo na endapo ataondoka basi atakuwa anasafisha njia ya pogba kutua Chelsea.
.jpg)
No comments:
Post a Comment