Chadema Yawasaidia Kutoka Mahabusu Vijana Waliotembea kwa Miguu Toka Geita Mpaka Dar Kumuona Rais



Chama cha Upinzani cha Chadema Imewasaidia Vijana watatu kutoka mahabusu Baada ya Kukamatwa na Jeshi la Polis Ijumaa iliyopita, Vijana hao walitembea kwa Miguu kutoka Geita mpaka Dar es salaam huku wakiwa wamevaa magunia kwa muda wa mwezi mmoja ili kuja kumshinikiza Rais Jakaya kikwete kutatua matatizo yanayowakabili wananchi na kutumia vitega uchumi vizuri kwa faida ya kila mwananchi

Safari ya hao vijana kutoka Geita iliishia mikononi mwa polisi baada ya kufika Dar bila kutimiza lengo lao la kumuona Rais kwa kili kinachosemekana kuwa hawakufuata utaratiba unaopaswa ili kuweza kumuona Rais wa nchi hiii, chama cha Chadema baada ya kuwatoa kimesema kitahakikisha haki yao inapatikana na kama watashtakiwa basi itachukua jukumu la kuwasimamia mahakamani..

Je Mdau  wa Udaku Una Maoni Gani Kuhusu Hao Vijana Waliotembea Muda wa Mwezi mmoja na Mwisho hawakuweza kutimiza lengo lao?


No comments:

Post a Comment

Peruzi Kurasa.

Designed By Seo Blogger Templates Published.. Blogger Templates