Brendan Rodgers: Nilitaka Steven Gerrard abaki Liverpool FC.

Brendan Rodgers amepuuza madai kuwa Liverpool FC haikufanya juhudi za kutosha kumbakisha Steven Gerrard katika uwanja wa Anfield.

Gerrard alitangaza siku ya Ijumaa msimu huu utakuwa mwisho wa miaka yake 25 ya kushirikiana na klabu wakati mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu.

kiungo huyo mkongwe anayetarajia kutimu miaka 35 hivi karibuni alipewa makataba mpya na Klabu hiyo lakini badala yake alisisitiza uamuzi wake wa kucheza soka nje ya uingereza ambapo klabu ya ligi kuu marekani, La Galaxy imeonesha nia ya kumtaka.
Na Rodgers anaamini Gerrard imefanya uchaguzi kulingana na maisha na nia yake ya kuendelea kucheza soka mara kwa mara
"Taarifa ya Steven iko wazi," alisema bosi Reds. "Anajua hisia zangu kuhusu nini alikuwa akifanya hapa. Yeye amekuwa nahodha mwenye kipaji kwa  muda wangu wote hapa.




No comments:

Post a Comment

Peruzi Kurasa.

Designed By Seo Blogger Templates Published.. Blogger Templates