Avril na Ommy Dimpoz Wanapendeza pamoja.

Avril ameufungulia mwaka wake ndani ya Bongo ambapo amekuwa karibu sana na Mkali Ommy Dimpoz wakiwatengenezea mashabiki wao kitu kikali.

Intaneti na mitandao ya kijamii kwa ujumla imejaa picha za wawili hao wakifurahia wakati wao pamoja kwa kile wanachokiita ni maandalizi ya single yao mpya iliyowachukua miaka mitatu kukamilika.

Lakini hata kama tutaamini kile ambacho hawa waburudishaji wetu wanachokisema, hufikiri kwamba Avril na Ommy Dimpoz wanapendeza pamoja?

Tizama picha hizi ambazo Avril ametupia katika akaunti yake ya instagram. Muda mwingi pamoja katika saluni na mengine mengi yanatueleza zaidi.

Lakini usiogope. wawili hao wanaufanyia kazi wimbo wao mpya wanaosema utatoka hivi karibuni. kitu kimoja cha kuaminia, wimbo huo utasumbua! Ommy Dimpoz, kama vile Diamond, huwa hawatuangushi. Vilevile Avril. 




No comments:

Post a Comment

Peruzi Kurasa.

Designed By Seo Blogger Templates Published.. Blogger Templates