Binti mmoja raia wa Poland aliwashangaza jopo la madaktari waliokuwa wanamfanyia upasuaji maalum katika sehemu ya ubongo wake, baada ya kuamka wakati upasuaji ukiendelea na kuwauliza madaktari namna upasuaji ulivyokuwa ukiendelea, gazeti la Daily mirror linaripoti.
Iga Jessica (19) amekuwa akifanyiwa upasuaji maalum kuondolewa kansa iliyokuwa inajitokea ndani ya ubongo wake. Madaktari wanasema kwamba Jessica aliamka baada ya ganzi aliyopigwa kuisha,japokuwa ubongo wake ulikuwa nje hakuweza kuathirika.
Pamoja na kuamka kwake, Jessica hakuweza kuhisi chochote na wala hakuwa hatarini, hakuweza kuona wala kuhisi chochote na wala hakumbuki kama aliamka wakati wa operesheni.
Madaktari bado wanachunguza huenda ganzi aliyochomwa binti huyo haikumwingia sawasawa ingawa wataalamu wengine waliliambia Daily Mirror kuwa operesheni yenyewe ilikuwa na uwezo wa kumwamsha bila kujali ganzi.

No comments:
Post a Comment